Kocha Mkuu wa Young Africans, Miguel Gamondi amefichua licha ya mabosi wa timu hiyo kukamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji Augustine Okrah raia wa Ghana, lakini bado anataka kuona anapata mshambuliaji halisi wa kati ili kufikia malengo katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mpaka sasa katika usajili wa dirisha dogo, Young Africans wamefanikiwa kutambulisha wachezaji wawili ambao kiungo wa kati, Shekhan Ibrahim kutoka JKU ya Zanzibar na Mghana, Augustine Okrah kutoka Bechem United.

Young Africans inahusishwa na washambuliaji mbalimbali kama Mcameroon Leonel Ateba, Simon Msuva, Jonathan Sowah raia wa Ghana na hawa wote wameitwa kwenye timu zao za taifa ambazo zitashiriki Fainali za Mataifa ya Afrika ‘AFCON 2023’.

Gamondi amesema kuwa anatambua ukubwa na ubora wa kiungo huyo na anaamini ataongeza kitu ndani ya timu yake lakini bado anahitaji la mshambuliaji halisi wa kati kutokana na ugumu wa mashindano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika wanaoshiriki.

“Okrah ni mchezaji mzuri, ataongeza kitu ndani ya timu yangu hasa eneo la mbele na jambo muhimu ni kwamba ameshacheza hapa na anajua mazingira na kitu gani anapaswa kufanya, naamini atatusaidia sehemu kubwa.

Lakini bado naona tunahitaji kuona tunapata mshambuliaji wa kati ambaye ni halisi ili kuweza kufikia malengo katika michuano ya kimataifa kwa sababu uhitaji wetu katika hilo ni mkubwa na viongozi wanatambua nini ambacho tunahitaji kufanya ili kufikia malengo.

Ndidi kuzikosa fainali za AFCON 2023
Mbappe: Siijui hatma yangu PSG