Afarah Suleiman, Hanang’ – Manyara.

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Cuthbert Sendiga leo Januari 4, 2024 amefika kijiji cha Gendabi Wilayani Hanang’ kusikiliza maoni ya Wananchi na kueleza jitihada za Serikali zinazoendelea katika kuhakisha wanarudisha maisha ya kawaida Wilayani humo.

Akizungumza na Wananchi hao, ukiwa ni mkutano wake wa kwanza tangu kuanza kwa mwaka 2024, Sendiga amesema tayari Serikali imetenga eneo na na kupima viwanja zaidi ya 200 kwa ajili ya ujenzi wa Nyumba za makazi 89, Zahanati na huduma nyingine za kijamii.

Amewataka Wananchi wa Gendabi kuwa wamoja na kushikamana kwa wakati wote, jambo ambalo liliungwa mkono na Wananchi wakiwemo waathirika wa Maporomoko hayo.

Hata hivyo, bado mashirika ya umma, Taasisi mbalimbali za Serikali, Wananchi na Viongozi wa Dini wameendelea kufika eneo hilo kutoa pole na kuwashika mkono waathiriwa.

Kiungo mpya Simba SC aaga rasmi
Ndidi kuzikosa fainali za AFCON 2023