Klabu ya Coastal Union imeachana na Mlinda Lango wake Justine Ndikumnana, raia wa Burundi ambaye amekuwa mchezaji wa nane kuachwa ndani ya timu hiyo kwenye dirisha hili la usajili, ambalo linatarajia kufungwa Januari 15.
Wachezaji wengine ambao wamepewa mkono wa kutokea na Coastal Union ni Konare, Abdulswamad Kassim, Daud Mbweni, Yakub Abdullah, Fran Golubic, Juma Mahadhi na Juma Mahadhi.
Ofisa Habari wa Coastal Union, Abbas El Sabri, amesema lengo ni kuboresha kikosi chao na wachezaji wanaoondoka kwenye kikosi hicho hawapo kwenye mnipango ya kocha mkuu.
Tunataka kutumia dirisha hili kuimarisha kikosi ili tuweze kutimiza malengo yetu ambayo tulijiwekea tangu mwanzo wa msimu.
“Kuondoka kwa wachezaji hawa ni kuruhusu tufanye usajili mwingine ambao utaenda kuongeza wachezaji wapya ambao watakuja kuleta kitu kipya kwenye kikosi chetu,” amesema El Sabri.
Amesema kamati ya usajili imeendelea kufanya usajili na wakati wowote wataanza kutambulisha nyota wapya ambao wataongeza nguvu kwenye kikosi cha kocha David Ouma raia wa Kenya.