Mshambuliaji Mmkongwve wa Ghana, Andre Ayew ana matumaini ya kuweka rekodi moja na kuifikia nyingine wakati wa Fainali za Mataifa ya Afrika ‘AFCON 2023’ nchini Ivory Coast kuanzia Jumamosi (Januari 13).

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34, ambaye hivi kariburi alijiunga na klabu ya Ligi Kuu ya Ufaransa ya Le Havre, na lengo lake kuwa mchezaji wa kwanza kufunga katika mashindano saba ya Afrika.

Rekodi yake ya kufunga mabao sita anaishikilia pamoja na Mghana mwenzake Asamoah Gyan, Mzambia Kalusha Bwalya na Mcameroon Samuel Eto’o, wafungaji hao wa muda wote wakiongoza kwa kufunga mabao 18 katika fainali za AFCON.

Pia ana matumaini ya kuwa nyota wa tatu kucheza mashindano nane, ambayo yalianza kuchezwa mwaka 1957 yakiwa na nchi tatu, lakini sasa yana washiriki 24.

Rigobert Song, ambaye ataifundisha nchi yake ya asili Cameroon katika fainali za mwaka huu, na Mmisri Ahmed Hassan wanashikilia kwa pamoja rekodi ya kushiriki mara nyingi mashindano hayo.

“Kipaumbele changu ni kuanza au kutokea benchi katika mashindano ya Ivory Coast, “amesema Ayew alipozungumza na waandishi wa habari kuelekea mchezo wa Kundi B dhidi ya Cape Verde, pamoja na Misri mabingwa wa kihistoria na Msumbiji.

Ghana ndio timu inayoshika nafasi ya tatu kwa mafanikio katika mashindano hayo baada ya Misri na Cameroon, ikishinda mara nne lakini kwa mara ya mwisho ilitwaa taji mwaka 1982 wakati walipowafunga wenyeji Libya katika fainali iliyoamriwa kwa Penati.

Wamemaliza wa sita mfululizo kuanzia mwaka 2008, lakini waliangukia katika raundi ya 16 miaka mitano iliyopita na walipata kipigo kikubwa baada ya kutolewa katika raundi ya kwanza mwaka 2022 baada ya kufungwa na vibonde Comoro.

Kocha Nigeria aahidi makubwa AFCON 2023
Justine Ndikumnana aondoka Coastal Union