Afarah Suleiman, Hanang – Manyara.
Mkuu wa Mkoa Manyara, Queen Sendiga amewataka Maafisa Elimu Kata na Wilaya kuhakikisha wanafunzi wote wanafika shule kuanza masomo ifikapo January 10, 2024 na baada ya hapo wasiofika wachukuliwe hatua za kisheria.
Sendiga ametoa maelekezo hayo leo January 8 alipotembelea Shule za msingi na Sekondari zilizoathiriwa na Janga la maporomoko ya tope na mawe katika mji wa Katesh, uliopo Wilayani Hanang mkoani humo.
Akiwa katika Shule ya msingi Jorodom ambayo ilipoteza wanafunzi 15 katika Janga Hilo, Sendiga ameelekeza uongozi wa shule hiyo kuorodhesha wanafunzi wenye changamoto ya sare kutoka familia zilizoathiriwa ili wasaidiwe mahitaji hayo muhimu Kwa haraka.
Serikali, imekuwa ikihimiza suala la elimu kwa kila mtoto, ambapo suala hilo pia limekuwa likitiliwa mkazo na kusisitizwa na Wadau mbalimbali zikiwemo taasisi binafsi na Wananchi.