Kocha Mkuu wa Chelsea Mauricio Pochettino ametoa maoni machache alipoulizwa kuhusu uwezekano wa The Blues kutaka kumsajili kiungo wa kati kutoka Ligi Kuu ya Saudia, Jordan Henderson, baada ya timu yake kushinda 4-0 kweye FA dhidi ya Preston mwishoni mwa juma lililopita.
Mchezaji huyo wa Kimataifa wa England alizua utata alipoondoka Liverpool na kuelekea Mashariki ya Kati wakati wa majira ya joto na inasemekana hana furaha na maisha katika klabu mpya ya Al Ettifaq.
Henderson mwenye umri wa miaka 33, amebakiza nafasi yake katika kikosi cha England cha kocha, Gareth Southgate licha ya kuhamia Saudi Arabia.
Alisema: “Hatukuzungumza kuhusu majina. Kwa sasa, hatuzungumzii kuhusu wachezaji.
“Nilimwona Behdad (Eghbali), akiwa na Paul (Winstanley) na Laurence (Stewart). Nadhani tutakuwa na mazungumzo. Hatukuzungumza kuhusu majina au wachezaji. Kwa sasa tunaangazia wachezaji kama Andrey Santos.
Henderson ni gwiji wa Anfield, akiwa nahodha wa Wekundu hao kwa mafanikio katika Ligi Kuu, Ligi ya Mabingwa Ulaya, Kombe la FA na Kombe la Carabao kabla ya kutumia muda wake wa miaka 12 kucheza pale Merseyside.