Mahakama ya Shanzu ya Nchini Kenya huenda ikamuachilia kwa dhamana mshukiwa mkuu wa mauaji ya Shakahola, Paul Mackenzie na wenzake.

Taarifa za kuachiliwa huru kwa Mackenzie na wenzake, zinadaiwa huenda zikatekelezwa iwapo Serikali itashindwa kuwafungulia mashtaka.

Mahakama hiyo, kwasasa imesema imeamua Mackenzie na washukiwa wenzake kuendelea kuzuiliwa kwa siku 14 zaidi, ili kutoa muda kwa Serikali kuchukua hatua.

Hatua hizo ni pamoja na kuwafunguliwa mashtaka watuhumiwa hao au iwaachiliwe kwa dhamana hadi pale upande wa mashtaka utakapokuwa tayari kufanya hivyo.

Zaidi ya 6,000 wafariki wakijaribu kwenda Ulaya
DC Twange atangaza msako wa nyumba kwa nyumba