Afarah Suleiman, Babati – Manyara.
Katibu wa Halmshauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi – CCM, Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Paul Makonda anatarajia kufanya ziara ya kikazi Mkoani manyara akiwa akitokea Mkoani Arusha, ambapo Wananchi wametakiwa kujitokeza, ili kuelezea changamoto zinazowakabili.
Hayo yamebainishwa na Katibu wa Siasa Uenezi na Mafunzo w CCM Mkoa wa Manyara, John Nzwalile wakati akiongea na Waandishi wa Habari ofisini kwake na kusema Kiongozi huyo anatarajia kupokelewa katika Kata ya Magugu, Mkoani humo.
Amesema, baada ya kufika Mkoani Manyara atafanya mkutano wa hadhara katika viwanja vya Stendi ya zamani na kusikiliza kero mbalimbli za Wananchi wa maeneo yote ya Mkoa wa Manyara.
Katika hatua nyingine Nzwalile amewaonya Viongozi wasio wajibika na kusababisha migogoro ya ardhi Kwa Wananchi katika maeneo mbalimbali Mkoani humo akisema CCM inawataka kuwajibika na kuacha na kuondoa migogoro hiyo mara moja.
Kuhusu uchaguzi wa Serikali za mitaa, Nzwalile amewakemea wale wanaopanga safu ya Viongozi wanaowataka wao na sio Wananchi na kusema endapo jambo hilo litabainika hatua kali zitachukuliwa kwa mujibu wa taratibu za chama.