Uongozi wa Young Africans umesema kuwa baada ya kutolewa katika michuano ya Kombe la Mapinduzi inayoendelea kutimua vumbi visiwani Zanzibar, sasa wanahamishia hasira zao zote kwenye mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika dhidi ya CR Belouizdad ya Algeria.
Young Africans katika mchezo wao unaofuata wa Ligi ya Mabingwa wanatarajiwa kucheza na Waarabu hao kutoka Algeria Februari 25, mwaka huu jjini Dar es salaam.
Ofisa Habari wa Young Africans, Ally Kamwe amesema kuwa: “Kwa sasa tumetolewa katika michuano ya Mapinduzi tunachukuwa nafasi hii kuwaomba radhi mashabiki wetu wote ambao walikuwa wanatarajia kutuona tunafika mbali zaidi ya hapa.
“Kwa sasa tunaangalia michezo yetu inayofauta ile ya Ligi Kuu na ile ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika ambapo tutakuwa na kibarua mbele ya CR Belouizdad, tunataka kuhakikisha kuwa tunapata matokeo ya ushindi dhidi yao.
“Hivyo tutakuwa na muda mzuri wa kupumzika, lakini pia muda mzuri wa kujiandaa ili tuweze kupata maandalizi mazuri ya kufanya vyema katika mchezo huo,” amesema Ally Kamwe.