Timu ya taifa ya Morocco iko katika presha kubwa kuhakikisha inakuwa na kiwango cha juu katika Fainali za Mataifa ya Barani Afrika ‘AFCON 2023’ kama ilivyokuwa ‘moto’ wakati wa Fainali za Kombe la Dunia miezi 2022 nchini Qatar.

Morocco katika Fainali za Kombe la Dunia Qatar iliweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza kutoka Barani Afrika kucheza hatua ya Nusu Fainali, huku timu hiyo ikianza kwa sare dhidi ya Croaria katika mchezo wa Kundi F.

Fainali za ‘AFCON 2023’ inatarajia kuanza kutimua vumbi kuanzia Jumamosi Januari 13 na kumalizika Februari 11, mwaka huu.

Baada ya kufikia hatua ya Nusu Fainali ya Kombe la Dunia sasa inataka kupeleka makali yake katika ‘AFCON 2023’.

Morocco ni moja ya nchi 12 kati ya 24 zinazocheza mashindano hayo ya Afrika ambazo ziliwahi kutwaa taji la Afrika, lakini nchi hiyo kwa mara ya mwisho ilitwaa taji mwaka 1976.

Wana historia ndefu tangu walipotupwa nje ya mashindano wakati walitarajiwa kufanya vizuri.

“Ni kweli kuwa fainali zilizopita za Kombe la Dunia zimetupa uzoefu wa kutosha katika mashindano makubwa lakini kwetu ukweli ni kwamba Kombe la Mataifa ya Afrika wakati wote ni mashindano yenye utata,” amesema kocha Walid Regragui.

“Hii sio mara ya kwanza Morocco inawasili ikiwa timu inayopewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa, lakini bahati mbaya hatukufanikiwa kuwa timu ambayo mara zote inamaliza katika nne bora.

“Hiyo inaonesha kuwa pamoja na uzoefu wa mashindano, hiyo sio sababu kubwa ya kutuhakikishia sisi ushindi.”

Kocha huo alisema kuwa wanatarajia upinzani mkali kutoka kwa wenyeji Ivory Coast, Ghana, Nigeria na mabingwa watetezi Senegal.

Riyad Mahrez : Tunajua maana ya AFCON
Sadio Mane: AFCON 2023 kuna kazi nzito