Johansen Buberwa, Bukoba – Kagera.

Mkuu wa Wilaya Bukoba, Erasto Sima ametangaza kuanza Msako wa Nyumba kwa nyumba wa kutafuta Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2024 Wilayani humo ambao hawajaripoti Shule.

Akizungumza na Wananchi wa Kata ya Kashai wakati wa ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo, kusikiliza na kutatua kero amesema hali ya Wanafunzi kuripoti Shule katika kata hiyo hairidhishi tangu zilipofunguliwa.

Sima pia amesema idadi ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza katika shule ya Sekondari Samia Hassan ni 98 na walio ripoti hadi leo Januari 11, 2024 ni 24 pekee wavulana wakiwa 14 na wasichana 10.

Amesema, Shule ya Sekondari Kashai idadi ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kwa mwaka huu ni 550 na walio ripoti na kuanza masomo Wavulana ni 148 na Wasichana 157 na kufanya jumla ya Wanafunzi 305 sawa na asilimia 54.4.

Zaidi ya Mabati 1,000 ya TAHOA yakabidhiwa Hanang'
Bruno Gomez aisononesha Singida FG