Serukali ya Burundi imetangaza kufunga mpaka wake na Rwanda, ikiwa ni muda wa wiki mbili tangu kuituhumu nchini hiyo kuunga mkono waasi waliofanya mashambulizi kwenye ardhi yake.

Burundi inasema kundi la Waasi la RED-Tabara lilifanya shambulizi Desemba 22, 2023 karibu na mpaka na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na kuuwa watu 20, wakiwemo Wanawake na Watoto.

Tangu kutokea kwa shambulio hilo, Rais wa Burundi, Evariste Ndayishimiye amekuwa akiituhumu Rwanda kuwaunga mkono waasi hao, madai ambayo serikali ya Rwanda imeyakanusha huku ikisema ufungaji wa mpaka unakiuka masuala ya ushirikiano.

Awali, Waziri wa mambo ya ndani wa Burundi, Matin Nitereste alisema wameamua kufunga mpaka wao na Rwanda na kuituhumu Rwanda kuwa inawahifadhi wahalifu wanaowadhuru watu wa Burundi.

Polisi yawadaka 21 kwa uhalifu wa mtandao
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Januari 12, 2024