Wakazi wa Kijiji cha Mpirani kilicho eneo Bunge la Magarini Kaunti ya Kilifi, wameelezea hofu yao juu ya ongezeko la Watoto wanaozaliwa na ulemavu katika miaka ya hivi karibuni.

Hofu hiyo, imezidi kutawala miongoni mwao  licha ya utafiti wa afya kutoka Serikali ya Kitaifa – DHS ya mwaka 2022, kudai kuwa kina mama katika eneo bunge la Magarini hawahudhurii kliniki wanapokua waja wazito na baadhi yao hujifungulia nyumbani.

Hata hivyo, wengi wao wamedai kwasasa Watoto wengi wamekuwa wakizaa Watoto wenzao na wanashindwa kuwa wakweli i wapate usaidizi na kujua taratibu husika za uzazi, huku wakihangaika na mitindo ya maisha na si kujali taratibu za ujauzito.

Wakati huo huo, Polisi katika eneo la Njukini Taveta kaunti ya Taita Taveta, wanamsaka mama mmoja, baada ya kuacha mtoto mchanga katika kibanda cha kuuza mboga katika soko la Njukini.

Mtoto huyo anayekadiruwa kuwa na mwezi mmoja, amepatikana akiwa kwa wachuuzi, kabla ya kupelekwa katika Zahanati ya Njukini kufanyiwa vipimo vya afya.

Ubakaji wampa miaka 30 jela Shaibu Makompyuta
Malawi inapoleta vibonzo vya sitaki nataka