Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Deogratius Ndejembi amemuagiza Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Adolf Nduguru kupeleka timu ya wakaguzi kukagua matumizi ya fedha kwenye ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Mkoa wa Mbeya ambayo ujenzi wake unasuasua.

Ndejembi, ametoa agizo hilo kwenye ziara yake ya kukagua ujenzi wa shule hiyo inayogharimu Sh. 3 Bilioni, ambapo inajengwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Kyela mkoani Mbeya.

Qlisema, “hapa hamjatendea haki fedha hizi zilizoletwa na Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya watoto wa kike wa Mkoa wa Mbeya. Fedha hizi zilipokuja ni kama fedha zingine za shule ilitakiwa baada ya kuingia tu mzihamishie kwenye akaunti ya shule na siyo kubaki nazo kwenye akaunti ya Halmashauri ili kuepuka changamoto za mifumo ambazo wataalamu wenu wanajaribu kuzieleza.”

“Mngeweza kuhamishia fedha hizi kwenye akaunti hata ya shule jirani kama wenzenu sehemu zingine walivyofanya na leo msingekuwa mnaongelea changamoto ya mifumo lakini nyie mkaamua kuzihodhi fedha hizi. Sasa nimuelekeze Katibu Mkuu TAMISEMI kutuma timu ya wakaguzi kuja kuchunguza ujenzi wa shule hii ili tuweze kuchukua hatua stahiki haraka,” aliongeza Ndejembi.

Aidha amemtaka Mhandisi wa mradi huo kusimamia masharti ya mkataba wa ujenzi huo kwa kuhakikisha mkandarasi aliyepo analeta idadi ya mafundi wanaotakiwa kisheria na kukamilisha haraka ili wanafunzi wa kike wa mchepuo wa sayansi wa mkoa wanufaika na matunda ya serikali yao.

Ufadhili Sekta ya Afya watarajia kushuka
Afisa wa Benki Mahakamani kwa kumuibia Mteja