Waziri wa Afya wa Uganda, Jane Aceng amesema ufadhili wa sekta ya afya unatarajiwa kushuka kwa asilimia 49, huku msaada wa wa Taifa hilo kutoka kwa wafadhili ukitarajiwa pia kupungua kutoka dola 732,963,975 mwaka 2023/24 hadi dola 7,627,464.02 ya bajeti ijayo ya mwaka 2024/25.
Akiongea mbele ya Kamati ya Bunge, Aceng pia alikataa kuhusisha kushuka kwa ufadhili nhuo a kupitishwa kwa sheria ya kupambana na mapenzi ya jinsia moja ya Mei 2023.
Alisema, “ufadhili umekuwa ukishuka na nimekuwa nikiwasilisha hili kwa sababu wafadhili hawawezi kutuunga mkono milele. Kweli, hivi majuzi, tulisikitishwa pale PEPFAR ilipotangaza kujitoa, kukawa na mjadala mzito kwenye baraza lao la mawaziri.”
Bunge la Uganda, lilipitisha marekebisho ya Sheria ya Kupinga mapenzi ya jinsia moja Mei 2023 na serikali ya Marekani ikatishia kuondoa ufadhili kwa Uganda kupitia Mpango wa Rais wa kupambana na Ukimwi, PEPFAR.