Familia moja katike eneo la Mtwapa Nchini Kenya, imelazimika kumpeleka mgonjwa wao anayepumulia mashine katika ofisi za Kenya Power, wakidai ukosefu wa umeme kwa muda mrefu katika mtaa wao ni hatari kwake.
Familia hiyo yenye asili ya bara la Ulaya, imesema uamuzi wao unatokana na kuona ukosefu wa umeme unahatarisha maisha ya mgonjwa wao, ambaye anapaswa kutumia mitambo inayohitaji umeme kupumua.
Wamesema, wanahitaji pia kufahamu kiini cha kupotea kwa umeme kila mara katika eneo lao, kwani hiyo imesababisha maisha yao kuwa magumu kutokana na shughuli nyingi za kiutendaji ndani mwao kukwaama.
Kukatika kwa Umeme, kumekuwa na athari kwa mataifa mengi ya Bara la Afrika, kukitokana na sababu mbalimbali ikiwemo uchakavu wa miundombinu, uhaba wa maji katika mabwawa yanayosaidia uzalishaji nk.