Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Beno Malisa amewataka Wananchi kuendelea utamaduni wa kuliombea Taifa amani na utulivu, kwani hawana Nchi nyingine zaidi ya Tanzania

Malisa ameyazungumza hayo Kanisa la Efatha lililopo Jijini Mbeya huku pia akiwakumbusha waumini wa kuliombea amani na utulivu Taifa na Viongozi waliopo wakiongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.

Kwa upande wake Mchungaji wa Kanisa hilo, Phillipo Mollel amesema wao kama watumishi wa Mungu, wataiombea Nchi na Viongozi ili waingoze Nchi, kwa hekima na busara.

 

Wachezaji Simba SC watimkia Mtibwa, KMC
Bondia Kidunda kusaini kimya kimya