Waziri wa Madini, Antony Mavunde amewataka wachimbaji wadogo kufuate sheria za uchimbaji na kuendelea kuchukua taadhari za kiusalama, katika migodi midogo.

Mavunde ametoa kauli hiyo wakati alipotembelea Mgodi wa Ng’alita uliopo Wilayani Bariadi mkoani Simiyu wakati akitoa salamu za pole kwa wachimbaji wadogo na kwa manusura wa ajali hiyo.

Aidha, alizipongeza Kamati za usalama kwa jitihada za uokoaji wa miili ya marehemu zaidi ya 21 ambao walifukiwa na ardhi wakati wanaendelea na shughuli za uchimbaji katika Mgodi huo.

Kufuatia tukio hilo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan alitoa salam za rambirambi kwa wafiwa na Taifa kiujumla kutokana na vifo hivyo vya watu zaidi 21.

Wawili wamfuata Francis Baraza Dodoma Jiji
Wachezaji Simba SC watimkia Mtibwa, KMC