Wanachama wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Nchini – TALGWU, wametakiwa kuwa Walinzi wa haki za wafanyakazi miongoni mwao, kwa kuzingatia dhana ya haki na wajibu na kutakiwa kujiepusha na vitendo vinavyoenda kinyume na misingi na maadili ya Utumishi wa Umma.

Wito huo, umetolewa na Naibu Waziri Wa Nchi, Ofisi Ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira Na Wenye Ulemavu, Patrobas Katambi wakati akizungumza kwenye ufunguzi wa kikao cha Baraza kuu la TALGWU Taifa, jijini Dodoma.

Amesema. “endapo wafanyakazi hawatajiepusha na matendo hayo maovu basi watafanya kazi ya kutetea na kulinda haki zao kuwa ngumu kwao na wadau wengine kama sisi. Lazima wakati wote tukumbuke kuwa kudai haki kunaenda sambamba na kutimiza wajibu.”

Naye katibu Mkuu wa TALGWU, Rashid Mtima ameiomba Serikali kushughulikia malalamiko ya watumishi wa kada ya Afya ya kutakiwa kujilipia ada ya leseni ya kila mwaka, huku wakiwa wanatekeleza majukumu ya kutoa huduma kwa umma.

“Na iwapo watashindwa kulipa ada hiyo wanakosa haki ya kupandishwa madaraja na kushindwa kubadilishwa vyeo, na ikumbukwe kuwa watumishi hawa hawafanyi biashara kwa leseni hizo isipokuwa wanatekeleza majukumu yao ya kilasiku kwa maendeleo ya taifa,” amesema Mtima.

Idadi ya Wagonjwa wa Kipindupindu imepungua - DC Sima
Pochettino apotezea usajili Chelsea