Johansen Buberwa – Bukoba.
Idadi ya wmWagonjwa wa Kipindupindu katika Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera, imepungua kutoka wanne hadi kufikia wawili, ambao ni wale waliokuwa wakipatiwa Matibabu kwenye Hospital ya Nshambya.
Mkuu wa wilaya Bukoba, Erasto Sima amesema kwa kwa sasa wagonjwa wawili waliobaki wanaendelea vizuri na kuwaasa wananchi kuzingatia usafi pamoja na kuchukua tahadhari dhidi ya Magonjwa ya mlipuko, ili waendelee kuwa salama.
“Vimelea bado vipo niwaombe wananchi muendelee kuchukua tahadhari ya kunywa maji yaliyochemshwa, vyakula vya moto na kabla ya kula tusafishe vizuri mikono kwa maji ya moto,” alisema Sima.