Kocha wa FC Bayern Munich, Thomas Tuchel, amesema Harry Kane ana uwezo wa kuvunja rekodi ya Robert Lewandowski ya msimu mmoja wa Bundesliga kufunga mabao 41, huku mshambuliaji huyo wa England akiendelea kufurahia msimu mzuri wa kwanza nchini Ujerumani.

Lewandowski aliweka historia Mei 2021 alipovunja rekodi ya msimu mmoja ya Gerd Müller,  ambayo ilidumu kwa miaka 39.

Kane alifunga bao lake la 22 la Bundesliga msimu huu katika dakika za mwisho za ushindi wa 3-0 wa Bayern dhidi ya Hoffenheim ljumaa (Januari 12) ingawa lazima afunge mabao 19 katika mechi 16 zilizosalia za Bayern ili kufikia rekodi hiyo.

“Iko hatarini,” Tuchel aliiambia ESPN alipoulizwa kama Kane anaweza kuvunja rekodi ya Lewandowski.

“Hakuna mtu ambaye angeweza.kuamini kwamba itakuwa hatarini, lakini iko hatarini.

Tunahitaji bahati kidogo. Tunahitaji timu kuendelea, Harry anahitaji kuwa fiti, na kisha tuone kile kinachokuja, kwa uwazi fikiria kwamba kwa Harry hakuna kikomo.”

Waziri Ndumbaro atoa nasaha Ivory Coast
Wachezaji Simba SC wapewa saa sita