Johansen Buberwa, Bukoba – Kagera.

Mkuu wa Wilaya Bukoba, Erasto Sima amevitaka vikundi vilivyokopa fedha za Serikali kupitia fungu la kumi la Mapato ya ndani kwenye Halmashauri ya Manispaa ya Vijana, Wanawake na Watu wenye Ulemavu kujesha haraka kabla msako wakuwatafuta haujaanza.

Akizungumza na Wananchi wakati wa ziara yake ya kusikiliza kero na kuzitatua kwenye kata 14 za Bakoba na Kitendaguro amesema vipo baadhi ya vikundi vimekopa fedha vimerejesha fedha kidogo na vingine havija rejesha kabisa.

Amesema katika Kata ya Bakoba vikundi 17 vilikopa kiasi cha shilingi milioni 98 tangu mwaka 2020 na kata ya Kitendaguro tangu mwaka 2019 idadi ya vikundi nane vilikopeshwa milioni 41 na zimelejeshwa milioni 24 na 84,000.

Bruno Guimaraes kung'oka kirahisi
Benchikha achekelea usajili Simba SC