Kiungo Mshambuliaji mpya wa Young Africans, Augustine Okrah, ameanza mazoezi ya viungo baada ya kukaa nje ya dimba kwa majuma mawili kufuatia kuumia katika mchezo dhidi ya KVZ, katika michuano ya Kombe la Mapinduzi.

Akizungumza Dar es salaam, Meneja wa Young Africans Walter Harrison, amesema Okrah amepona na ameanza mazoezi na wenzake na kujiweka fiti kwa michezo ijayo.

“Alipata majeraha makubwa, hali iliyosababisha kushonwa nyuzi kadhaa, kwa sasa yupo fiti na ameanza mazoezi,” amesema.

Amesema Young Africans imeanza maandalizi ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kutekeleza programu ya mazoezi ya viungo katika ukumbi wa Gymkhana kabla ya kurudi uwanjani.

Meneja huyo amesema Kocha Miguel Gamondi, ametoa ratiba ya mazoezi ya viungo ya juma moja kwa lengo la kuwapa nafasi wachezaji kuongeza stamina na pumzi.

“Wachezaji wote wapo mazoezini isipokuwa mshambuliaji mpya Joseph Guede, raia wa Ghana, ambaye tunatarajia atajiunga na timu wakati wowote,” amesema.

Hospitali mpya kujengwa kila Mkoa - Dkt. Mwinyi
Angola kuishangaza Afrika – AFCON 2023