Bertina Mangosongo – Zanzibar.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amezindua Chuo cha Wajasiriamali Wanawake Mkoa wa Kaskazini Unguja Cha Jumuiya ya Wanawake – UWT, ambacho ujenzi wake umegharimu Shilingi 72 Milioni.
Akizindua Chuo hicho, Rais Samia ameahidi kutoa Vyerehani vya Kisasa vitano kwa ajili ya kusaidia shughuli za kijasiriamali chuoni hapo.
Amesema, anawapongeza Viongozi wa UWT na wadau wote walioshiriki kuchangia mradi huo kwani utasaidia kutanua wigo wa ajira kwa kuwawezesha Vijana na Wanawake kujiajiri.
Rais Dkt Samia, pia amewataka Viongozi wa UWT kuendelea kusikiliza na kutatua changamoto mbalimbali zinazowagusa Wananchi ikiwemo kuhamasisha Wanawake kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika chaguzi zijazo.