Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba amekutana na Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje na Diaspora wa Jamhuri ya Kenya, Dkt. Musalia Mudavadi jijini Kampala.

Mawaziri hao, wamekutana Nchini Uganda pembezoni mwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi zisizofungamana na Upande Wowote (NAM) hii leo Januari 17, 2024.

Katika mkutano huo, wawili hao walijadili masuala mbalimbali ya kuimarisha ushirikiano baina ya Mataifa yao na kuahidi kuendelea kutumia majukwaa ya kidiplomasia kutatua changamoto mbalimbali.

Changamoto hizo ni pamoja na zile zinazokwamisha ustawi mzuri wa Biashara, uwekezaji, utalii na uendelezaji wa miundombinu kwa manufaa ya pande zote mbili.

Chelsea kumrudisha Ulaya Benzema
Wadakwa na Mil 13 bandia, mtambo wa pesa feki