Geita Gold iko kwenye maandalizi mazit0 ikijiandaa na mechi zijazo za Ligi Kuu na Komnbe la Shirikisho la Azam, ikiwa ikimbilia kujichimbia mkoani Morogoro ilikoweka kambi tangu Januari ll ikijifua vikali.
Kambi hiyo na baadhi ya wachezaji waliripoti kutoka mapumzikoni chini va kocha mkuu, Denis Kitambi na msaidizi wake, Charles Mlingwa huku winga wa timu hiyo, Yusuph Mhilu akitamba kutumia maandalizi hayo kurejesha ubora wake na kulishawishi benchi la ufundi kumpa zaidi nafasi ya kucheza.
Mhilu aliyejiunga na Geita mwanzoni mwa msimu huu akitokea Kagera Sugar, amebakiza miezi sita katika mkataba alionao na timu hiyo, huku akiandamwa na majeraha yaliyomuweka nje kwa muda mrefu.
Mhilu aliyewahi kukipiga Simba SC, amesema kwa sasa yuko fiti na kambi hiyo itamsaidia kuimarika zaidi chini ya kocha Kitambi na anaamini atapata muda wa kutosha kuelewa falsafa za kocha na kupata muunganiko na wachezaji wenzake.
“Tumeshaingia kambini, kambi yetu tumeiweka Morogoro tunasubiri tarehe ipangwe ya kurejea ligi tujue tunacheza na kina nani, tupo hapa tangu ili tuwe tayari na tumeanza mapeama ili ratiba itakapokuja pia kocha apate muda wa kuijua tiIu,” amesema Mhilu.