Imefahamika kuwa wachezaji wapya wote wa kigeni waliosajiliwa katika dirisha dogo la msimu huu wamepewa mikataba migumu ya miezi sita yenye masharti mazito ya kuichezea timu hiyo.

Nyota hao wa kigeni waliosajiliwa katika dirisha dogo ni kiungo mkabaji Babacar Sarr na washambuliai Freddy Koublane na Pa Omar Jobe, ambao tayari wametambulisha na timu hiyo.

Mastaa hao wote tayari wapo nchini wakisubiria ratiba ya kuanza mazoezi ya timu hiyo, chini ya Kocha Mkuu Mualgeria Abdelhak Benchikha aliyekabidhiwa jukumu la kukinoa kikosi hicho kinachojiandaa na Ligi ya Mabingwa Barani Afika, Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’.

Mmoja wa mabosi kutoka ndani ya Bodi ya Wakurugenzi ya timu hiyo, amesema wachezaji hao kila moja amepewa mkataba wa miezi sita ya kumalizia msimu huu na siyo miwili kama ilivyozoelezwa.

Bosi huyo amesema kuwa lengo la kuwapa mikataba hiyo. ni kwa ajili ya kuona ubora wa kila mmoja katika ligi na michuano ya kimataifa na kama kocha asiporidhishwa nao, basi wataachana nao.

Amesema kuwa wamechukua maumuzi hayo. kwa kuhofia kutumia gharama kubwa kuvunja mikataba ya wachezaji hao, endapo itatokea hawakuridhishwa na viwango vya wachezaji hao.

Ameongeza kuwa yapo makubaliano mazuri waliyokubaliana nayo ambayo yameainishwa katika mikataba yao, ambayo hayawabani kuachana nao baada ya ukomo wa miezi sita waliyokubaliana ya kuachana.

“Ngumu kumpata mchezaji wa kiwango bora ambaye yupo huru kusajili katika dirisha dogo, wachezaji wote bora wana mikataba hadi mwishoni mwa msimu huu.

Tulichokifanya ni kuwapa mikataba hiyo ya miezi sita wachezaji wote wa kigeni, ambayo kama wakimshawishi kocha na benchi la ufundi, basi tutawapa mikataba mirefu.

Lakini kwa sasa tumewapa mikatabu hiyo nifupi, yenye sharti na kama wakionyesha kiwango bora tutawaongezea mingine ya kuendelea kubakia hapa Simba SC.” amesema bosi huyo.

TAMISEMI, UNICEF wajadiliana kuimarisha Afya ya msingi
Hayyuma ampa tano Rais Samia chaguo la Nchimbi