FC Barcelona na Atletico Madrid zimeingia kwenye vita dhidi ya timu nyingine nne kwa ajili ya kuiwania saini ya kiungo wa Manchester City ya England, Kalvin Phillips, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Phillips mwenye umri wa miaka 28, hatma yake kwenye kikosi cha Man City inatarajiwa kuamuliwa wiki hii ikiwa ataendelea kubaki hadi mwishoni mwa msimu ama ataondoka.

Mchezaji huyu ameomba kuondoka kwa sababu hapati nafasi ya kutosha ndani ya kikosi hicho hali inayotishia nafasi yake kwenye Timu ya Taifa ya England.

Ilanfya afichua kilichomrudisha Mtibwa Sugar

Awali klabu za Newcastle na Juventus zilitajwa kuwa miongoni mwa timu zilizoonyesha nia ya kutaka kumsajili kwa mkopo lakini Man City ilikataa na kudai inataka kumuuza mazima.

Mkataba wake wa sasa unamalizika 2028. Katika msimu huu Phillips amecheza mechi 10 za michuano yote na kufunga bao moja na kati ya hizo nne ndio za Ligi Kuu England ambazo karibia zote aliingia akitokea benchi.

Kocha Zambia aisukia mkakati Tanzania
Ilanfya afichua kilichomrudisha Mtibwa Sugar