Mshambuliaji wa Brentford, Ivan Toney, amesema anapanga kuchezea “klabu bora inayoshindania mataji,” na hajakata tamaa kuondoka katika klabu hiyo ya London Magharibi mwezi huu kutokana na kuhusishwa na uhamisho wa kutua Chelsea na Arsenal.

Katika mahojiano na Sky Sports, Toney pia alisema analenga kujumuishwa kwenye kikosi cha England kinachonolewa na Gareth Southgate kwa ajili ya michuano ya Ulaya msimu huu baada ya kumaliza adhabu ya kufungiwa kwa miezi nane kwa kukiuka kanuni za Kamari za FA.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27, ambaye mechi yake ya mwisho katika kikosi cha kwanza cha Brentford ilikuwa dhidi ya Liverpool mnamo Mei 6, mwaka jana, ameruhusiwa kufanya mazoezi na wachezaji wenzake tangu Septemba na alifunga hat-trick katika mechi ya kirafiki Southampton uliochezwa Januari 6, mwaka huu.

“Huwezi kamwe kutabiri ni wakati gani mwafaka wa kuhamia kwingine, lakini nadhani ni dhahiri nataka kuchezea klabu kubwa,” amesema.

“Kila mtu anataka kuchezea klabu kubwa, ambayo inapigania mataji, inaweza kuwa Januari hii au baadaye kwa klabu kuingia na kulipa fedha zinazofaa, nani anajua?

“Lakini lengo langu kuu ni kufanya kile ninachopenda kufanya uwanjani.” Toney alitambuliwa kama mraibu wa kamari baada ya kukubali ukiukaji wa sheria ya FA kuhusu kamari.

Alipoulizwa inakuwaje katika mtego wa uraibu, Toney alisema: “Nisingeweza kukuambia labda kama vile waraibu wengine.

Wakati mwingine, hutambui unachofanya kwa sasa. Wewe Etambua tu baadaye unafanya E kitu ambacho hupaswi kufanya.”

Rahma achochea ushindani wa Elimu Ijuganyondo
GST kuweka vipaumbele sita utekelezaji wa ajenda Vision 2030