Jeshi la Polisi Nchini, kwa kushirikiana Jeshi la Wananchi – JWTZ na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa – TAKUKURU Mkoa wa Tabora, wametembelea Vyuoni na Shuleni, kutoa elimu ya kutambua na kuwafichua wahalifu na uhalifu katika maeneo yao.

Akitoa elimu hiyo, Mkuu wa Polisi Jamii Mkoa wa Tabora, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, Evodius Kasigwa amewataka Wanafunzi wa shule za Msingi, Sekondari pamoja na Vyuo vilivyopo Manispaa ya Mkoa huo kubaini na kuzuia kwa kutoa taarifa sahihi zitakazosaidia kuzuia uhalifu katika mkoa wa Tabora.

Katika ziara hiyo, SSP Kasigwa pia alitoa elimu ya madhara ya ukatili na unyanyasaji kwa watoto pamoja na namna ya kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi juu ya vitendo vya kikatili watakavyofanyiwa watoto hao.

Aidha, Wanafunzi hao walipewa elimu kutoka JWTZ juu ya matukio na viashiria vya ugaidi kuanzia Majumbani, Mitaani na Shuleni huku wakitakiwa kutoa taarifa sehemu sahihi endapo wataona au kuhisi viashiria hivyo.

Kwa upande wa Maafisa kutoka TAKUKURU, aliwaelezea Wanafunzi hao namna rushwa inavyoweza kutumika, hasa katika kushawishi jamii kutekeleza suala zima la jambo hilo ambalo ni adui wa haki.

Zahera achekelea usajili wa Kagere
Wabunge wa CCM washindwa kuzuia hisia zao