Mahakama ya Washington, imeamuru jina la Rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump liendelee kubaki kwenye karatasi za kura ya uteuzi wa mgombea Urais, kwa Chama cha Republican.
Hukumu hiyo, ilisomwa na Jaji wa Kaunti ya Thurston, Mary Sue Wilson akisema Msimamizi wa uchaguzi wa Jimbo la Washington alitekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria, pale alipoyakubali majina yote ya Wagombea yaliyowasilishwa na vyama vya Siasa.
Aidha, Wapigakura waliweka zuio lao Washington wakidai Trump hafai kuwania urais kutokana na tukio la Januari 6, 2021 ambapo hotuba yake ilichochea wafuasi wake kulivamia jengo la bunge wakitaka kupinduwa kwa matokeo ya uchaguzi wa 2020.
Hata hivyo, Mabadiliko ya 14 ya katiba ya Marekani yanapinga mtu mwenye tuhuma za uasi kuongoza ofisi ya umma na tayari Trump amezuiwa kwenye majimbo mengine ya Maine na Colorado kuwania wadhifa huo wa Urais.