Lydia Mollel – Morogoro.

Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Judith Nguli amelipongeza Jeshi la Polisi kwa kuendelea kuwa karibu na Wananchi na kueneza sera ya Polisi Jamii.

Nguli ameyasema hayo akiwa mgeni Rasmi kwenye sherehe ya familia za Askari (Police Family Day), iliyoandaliwa na Maofisa wakaguzi na Askari wa Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro na kufanyika kwenye viwanja vya Halmashauri ya Wilaya hiyo

Amesema, “ni sherehe yangu ya kwanza kuhudhuria kwa mwaka huu na imefana sana, Niwapongeze kwa kuitendea haki kauli mbiu ya Mh. Rais Samia Suluhu Hassan ya kulitaka Jeshi la Polisi kuwa karibu na Wananchi.”

Kwa upande wake Mkuu wa Polisi Wilaya ya Mvomero, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, Boniface Mwakalagesye amesema sherehe hizi si za Polisi pekee bali na familia pamoja na jirani zao ili kuonyesha mshikamano wao ambapo wamekuja kufurahi pamoja baada ya kazi za mwaka mzima.

Naye Koplo wa Polisi Neema Mwanga, Mshiriki wa sherehe hizo hakusita kueleza jinsi alivyo furahi kusherekea na familia yake na  kuwataka viongozi wake kuendeleza utaratibu wa kuandaa sherehe hizo kila mwaka kwani inafanya mioyo yao kufarijika na kufanya kazi kwa morali ya hali ya juu.

 

AFCON itumike kufuatilia Watoto: Namayala
Papa Francis amualika Rais Samia Vatican