Mkaguzi Kata ya Igamba Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, John Namayala amewakumbusha Wazazi na Walezi kuwafuatilia watoto wao kama wanavyofuatilia mechi za mataifa ya Afrika AFCON2023 zinazoendelea nchini Ivory Coast.

Namayala aliyazungumza hayo katika uwanja wa Shule ya Msingi Mwanda Kijiji cha Wantanda Wilayani Mbozi alipohudhuria na kuangalia mechi ya Yank Star na Mapinduzi Fc iliochezwa Kijijini hapo na kuwakuta watoto waliokuwa wanafuatilia mechi hiyo wamepanda juu ya miti hali ambayo ni hatari kwa uhai wao.

Alisema “Wazazi na Walezi tumekuwa na mwamko mkubwa katika kufuatilia michezo hususani AFCON2023, sasa basi mwamko huko tuugeuzie kwa watoto wetu kwa kuwafuatilia kwa karibu mienendo ya michezo yao kwani katika michezo hiyo ucheza michezo hatarishi ambayo inaweza kuwasababishia ulemavu au kifo.”

Viongozi Wakuu China, Poland, Cuba kutembelea Tanzania
DC afurahia ukaribu wa Polisi, Wananchi