Bondia wa ngumi za kulipwa Seleman Kidunda amemwambia mpinzani wake, Asamahle Wellem raia wa Afrika Kusini kuwa akae akijua anakuja Bongo kupokea kichapo kizito ambacho kitakuwa ni kisasi kwa bondia Mtanzania, Twaha Kiduku aliyewahi kupoteza kwa Msauz huyo.

Kidunda anatarajia kupanda ulingoni Machi, mwaka huu kwenye Ukumbi wa Warehouse kuwania mkanda wa ubingwa wa mabara wa WBF ambao Wellem atakuwa akiutetea, huku mabondia wengine wanaotarajia kupanda ulingoni ni Jesca Mfinanga, Lulu Kayage, Salim Mtango na Nasibu Ramadhan chini ya Feyherous.

Kidunda amesema kuwa sababu kubwa ya kulikubali pambano hilo ni kutaka kulipiza kisasi kwa Mtanzania mwengine aliyepigwa na bondia huyo wa Afrika Kusini.

“Nashukuru kwa nafasi ya pambano hili kubwa, ninachotaka kumwambia mpinzani tayari nimesaini mkataba wa kumalizana na yeye hivyo asitarajie chochote zaidi kutoka kwangu zaidi ya kichapo, hana uwezo wa kunipiga.

“Binafsi nimeona namna anavyopigana na mara ya mwisho alimpiga ndugu yetu hapa sasa kwa nini tukubali kumuacha, ameshaingia kwenye mtego kinachosubiria siku ifike tumalize utata kabisa wa kulipiza kisasi chetu, ” amesema Kidunda.

Dkt. Biteko ampokea Naibu Waziri Mkuu wa China
Young Africans imedhamiria 2023/24