Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Elimu ya Afya kwa Umma, Wizara ya Afya Dkt. Tumaini Haonga amewataka Wananchi kuendelea kuchukua tahadhari za kiafya, ikiwemo kudumisha usafi wa mazingira katika maeneo yao ili kuzuia magonjwa ya mlipuko kutokana na Mvua zinazoendelea Nchini.

Dkt. Haonga ameyasema hayo jijini Dodoma na kuongeza kuwa mvua zinaponyesha kuna uwezekano wa athari za afya zinazoweza kujitokeza ikiwemo uharibifu wa miundombinu ya majitaka hali inayoweza kusababisha kusambaa kwa magonjwa ya mlipuko.

Amesema, “kutokana na Mvua zinazoendelea kunyesha,kuna athari za kiafya zinazoweza kujitokeza ikiwemo uharibifu wa miundombinu ya majitaka ambayo yanaweza kuchangia au kuibua kusambaa kwa magonjwa ya mlipuko kama vile ugonjwa wa Kipindupindu lakini kuongezeka kwa magonjwa yanayosababishwa na minyoo, homa ya matumbo.”

“Nitumie fursa hii kutoa wito kwa wananchi wenzangu na jamii kwa ujumla kwa kipindi hiki mvua zinaendelea katika maeneo mbalimbali wazingatie kanuni za afya kwa kudumisha usafi wa mazingira na kuepusha maji kutuama kwenye maeneo ya makazi”amesema.

Utabiri wa hali ya hewa uliotolewa na Mamlakaya Hali ya Hewa nchini, unaonesha kuwa upo uwezekano wa kuwepo kwa Mvua juu ya Wastani uwepo wa El Nino hadi Januari 2024, hasa katika mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Mara, Kigoma, Morogoro, Pwani , Dar Es Salaam, Tanga, Arusha, Manyara, na Kilimanjaro.

Kocha Mashujaa FC na mpango kazi
Henderson kusubiri kibali Uholanzi