Kuendelea kuwepo kwa muda mrefu kwa Wakimbizi na waomba hifadhi Nchini ni tishio kiusalama, kwani taarifa zilizopo zinaonesha wapo Wakimbizi na Waomba hifadhi ambao wameajiriwa Serikalini na wengine wamepewa teuzi katika nafasi zenye maamuzi.

Kauli hiyo imetolewana hii leo Januari 22, 2024 katika Mkutano wa saba wa CDF na Makamanda Jijini Dar es salaam na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Nchini, Jenerali Jacob Mkunda mbele ya Rais wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Amesema, “kuendelea kuwepo kwa muda mrefu kwa Waomba hifadhi na Wakimbizi hawa Nchini ni tishio la kiusalama kwani taarifa zilizopo ni kwamba baadhi ya Waomba hifadhi hao au Wakimbizi au Familia zao wameajiriwa Serikalini kwa nafasi mbalimbali na wengine wamepewa teuzi Serikalini katika nafasi zenye maamuzi.”

Aidha Mkunda ameongeza kuwa, Tanzania imekuwa ikipokea maombi ya Wakimbizi na Waomba hifadhi kutoka Burundi tangu mwaka 1972, Rwanda tangu mwaka 1994 na DRC tangu mwaka 1996, idadi ya Wakimbizi 27000 kutoka Burundi wa mwaka 1972 hawakuwekwa katika kambi za Wakimbizi badala yake Serikali iliamua kuwagawanya katika Vijiji 73 vilivyopo Mkoa wa Kigoma.

“Wakimbizi hawa na Familia zao bado wanaendelea kuishi katika Vijiji hivyo na kwa kutumia mbinu mbalimbali uhakikisha uzao wao
unapata Uraia wa Tanzania bila kufuata Sheria, Serikali ya Tanzania na Burundi zimekuwa zikiwashawishi Wakimbizi hao
kurejea Nchini mwao bila mafanikio,” alisema.

Vijana wadaiwa kujiunga na vikundi vya kigaidi
Kocha Mashujaa FC na mpango kazi