Nchi ya Cameroon imezindua mpango wa kwanza ulimwenguni wa chanjo dhidi ya Malaria katika hatua inayotazamiwa kuokoa maisha ya maelfu ya watoto kwa mwaka Barani Afrika.

Tayari Shirika la Afya Ulimwenguni – WHO, limeidhinisha chanjo hiyo ya RTS-S iliyotengenezwa kwa miaka takribani 40 na kampuni ya Uingereza ya GSK.

Muungano wa kimataifa wa chanjo Gavi, umesema Cameroon imekuwa nchi ya kwanza kutoa dozi kupitia mpango wa kawaida wa dozi ambao utatumiwa na nchi nyingine 19 baadae mwaka huu.

Hatua hiyo, inafuatia mafanikio yaliyopatikana katika majaribio yaliyofanyika kwenye nchi za Ghana na Kenya, ambapo takribani watoto milioni 6.6 katika nchi hizo watapatiwa chanjo hiyo ya Malaria kati ya mwaka 2024-2025 na zaidi ya nchi 30 kuonyesha nia ya kutoa chanjo hiyo.

Mikel Arteta awatia simanzi mashabiki
Mzize, Maxi wakumbuka VIBE la Wananchi