Idara ya afya katika kaunti ya Mombasa Nchini Kenya, imetaka wasimamizi wa shule za eneo hilo kuwa waangalifu na Wanafunzi wao, kufuatia kuzuka kwa maradhi ya macho, yajulikanayo kama macho mekundu au red eye disease.

Wito huo umetolewa na Afisa mkuu wa Afya wa Serikali Kaunti, Dkt. Salma Swaleh ambaye pia amewataka Walimu katika shule zote za maeneo Bunge, kuhakikisha Wanafunzi wanadumisha usafi kwa kuosha mikono mara kwa mara.

Aidha, amewataka pia kutogusa macho yao kwa mikono michafu, kufunika mdomo wanapokohoa au kucheua, ili kudhibiti maambukizi ya maradhi hayo ambayo yanaenea kwa kazi katika nchi za Afrika Mashariki.

Hivi karibuni, Serikali Nchini Tanzania kupitia Wizara ya Afya, pia iliwatahadharisha Wananchi wake kuwa makini na ugonjwa huo, huku baadhi ya walioathiriwa wakilalamikia kukosa kushiriki shughuli za kiuchumi.

Mtoto atolewa Skrubu kwenye Mapafu
MALIMWENGU: Dhihaka yenye kweli ndani yake