Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amemuagiza Naibu Katibu Mkuu, Sekta ya Mifugo, Prof. Daniel Mushi na Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera kuhakikisha kuwa maeneo yote yaliyopo katika Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO), Mkoani Kagera ambayo hayana mgogoro yatangazwe kwa ajili ya uwekezaji.

Ulega ametoa maelekezo hayo wakati wa kikao chake na Viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Kagera kilicholenga kumaliza migogoro iliyopo baina ya Wananchi na Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO).

Amesema, maeneo ambayo yameshapimwa na ambayo hayana mgogoro yatangazwe ili wawekezaji wenye uwezo waweze kupewa kwa ajili ya kufanya ufugaji wenye tija.

Aidha, amewataka Wataalam kurejea upya kwenye maeneo yote ambayo yameonekana yana migogoro ili kutatua changamoto zilizopo na kuwezesha maeneo hayo yaweze kuendelezwa na wawekezaji wenye uwezo.

MAKALA: Shoka moja ilivyoshusha Mbuyu chini
Dkt. Charles akagua utekelezaji mlipuko Kipindupindu