Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba amewasisitiza wafanya biashara kuendelea kulipa kodi ili kuendelea kujitengenezea mazingira mazuri ya kukuza biashara.
Akizungumza hii leo Januari 23, 2024 Jijini Dodoma katika uzinduzi wa Taasisi ya Usuluishi wa Malalamiko na taarifa za kodi, Majaliwa amesema taasisi hiyo itasaidia kuhamasisha zaidi Wananchi kulipa.
Amesema, “hizo kodi ndizo ambazo tunazitegemea katika kujenga barabara nzuri, shule za viwango, na huduma zote muhimu za kijamii ambazo ndio kidi hizo zinatumika katika kuleta maendeleo hayo, lakini mnapokuwa wazembe katika hayo tutakuwa kilasiku tunaona maendeleo kwenye Nchi za jirani”, amesema.
“Lazima tuwe na taifa linalojitegemea, siyo eshikakutegemea misaada kutoka Nchi za Jirani, kwaio ili tuepuke yote hayo ni lazima tukusanye mapato hili tufikie huko, na watu wetu wanaweza kulipa kodi bila mzozo ila ndio hivyo wanafanya makusudi,” alisema Nchemba.
Hata hivyo, amesema kuwepo kwa ofisi hiyo ya usuluhishi itasaidia kwenye suala la kukusanya mapato pamoja na kukuza uchumi na kuongeza kuwa “lazima tuhakikishe tunakuwa kiuchumi na tukiwa na malalamiko ya masuala ya kikodi inakuwa sio nzuri inaleta madhara sana kwa Nchi yetu, na itafanya tushuke kiuchumi, hivyo kupitia ofisi hii tunaimani kilakitu kitakuwa sawa na mtaendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya ulipaji kodi na kutoa risiti husika.”
Aidha, Nchema amesema, “Wenzetu huko walioendelea hawana masuala ya kukwepa kulipa kodi na ndiomaana kilasiku tunawatolea mifano kwasababu wanaendelea kiuchumi kilasiku, kwaio naimani na hii taasisi itabalansi uchumi wa Taifa letu.”