Kaimu Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania Hemed Morocco, amesema kuwa wana matumaini ya kupata matokeo kwenye mchezo wa leo Jumatano (Januari 24) dhidi ya DR Congo hatua ya makundi ili kufufua matumaini kutinga hatua ya 16 bora.

Ipo wazi kuwa pointi moja waliyopata Tanzania ilikuwa kwenye mchezo dhidi ya Zambia walifunga bao la mapema dakika ya 11 kupitia kwa Simon Msuva katika dakika za lala salama Zambia iliweka usawa na kufanya ubao kusoma 1-1.

Leo Jumatano (Januari 24), Taifa Stars inakibarua cha kusaka pointi tatu dhidi ya DR Congo iliyotoka kugawana pointi moja moja na timu ya Taifa ya Morocco ambayo iliifunga Tanzania mabao 3-0 kwenye mchezo wa kwanza hatua ya makundi.

Ikiwa Stars itapata ushindi leo itafikisha pointi nne, kama Zambia itapoteza dhidi ya Morroco angalau kutakuwa na nafasi ya kutinga 16 bora ikishinda matumaini yatayeyuka.

Morocco amesema: “Unaona namna ambavyo wachezaji wanacheza kila mchezo.  Hizi mechi zote ni ngumu tunarudi uwanjani kwa ajili ya kuwakabili DR Congo matumaini yapo na tuna nafasi ya kupata ushindi kwenye mchezo wetu ambao ni muhimu.

“Kwa kila timu ambayo ipo hapa ni hatua kubwa hakuna timu ndogo zote ni kubwa na ndio maana zinapambana. Tunajitahidi kwa uwezo wetu kuanzia wachezaji kila anayepata nafasi anaonyesha kuna kitu anahitaji. Makosa kwenye mchezo wetu uliopita tutafanyia kazi.”

Msuva amesema: “Tulijitahidi kwenye mchezo wetu dhidi ya Zambia kupata ushindi lakini ilishindikana kwenye mchezo wetu dhidi ya DR Congo tutajitahidi kushirikiana kupata pointi tatu muhimu zitakazotupeleka hatua inayofuata.”

Uboreshaji Miundombinu wageuka kero Mwembesongo
Kanuni zaibana Newcastle United