Uongozi wa Azam FC umeweka wazi kuwa utawashangaza wengi kwenye mwendelezo wa ligi kutokana na ubora wa kikosi kilichopo na wachezaji kuwa na shauku ya kufanya vizuri kwenye mechi za ushindani.
Ofisa Habari wa Azam FC Hasheem Ibwe, amesema kuwa ambacho wanakihitaji ni kuwa kwenye kasi ileile waliyoanza nayo kwa kupata ushindi na burudani kuwapa mashabiki zao.
“Tulikuwa kwenye mwendo mzuri kwenye ligi na matokeo yalikuwa yanaonekana uwanjani, unaona hata wachezaji bora hivi karibu walitoka ndani ya Azam FC na kocha bora pia kwa hiyo, huo ulikuwa ni mwendo mzuri.
“Kwenye mechi zijazo tunahitaji kuendelea kuwashangaza wengi ambao wanafikiria kwamba tutakuwa tumepoteza ile nguvu hilo litakuwa ni jambo jingine kabisa tupo kwa ajili ya kuendeleza ushindani,” amesema Ibwe.
Azam FC ni vinara wa msimamo kwenye ligi wakiwa nafasi ya kwanza baada ya kucheza mechi 13 wakiwa na pointi 31.