Makamu wa Rais wa Kamati ya Olimpiki Tanzania ‘TOC’, Henry Tandau ameliita Shirikisho la Soka nchini ‘TFF’ mezani kuelekea maandalizi ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika ‘AFCON 2027’ itakayoandaliwa na Tanzania, Kenya na Uganda.
Safari ya timu ya soka ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kwenye mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika, Ivory Coast ilifikia tamati juzi Jumatano (Januari 24) baada ya kutoka sare ya bila ya kufungana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na kushika mkia kwenye Kundi F ikiwa na pointi mbili.
Tandau akizungumza jijini Dar es salaam amesema fainali za Ivory Coast kwa Taifa Stars zimefikia tamati na muhimu kwa TFF kuona namna gani wanajiandaa kwa mashindano hayo ambayo Tanzania itaandaa kwa kushirikiana na Kenya na Uganda mwaka 2027.
“Sisi kama Kamati ya Olimpiki tuko tayari kushirikiana na TFF kama wadau muhimu kuelekea michuano ya Kombe la Fainali ya Mataifa ya Afrika ambayo Tanzania tutaandaa kwa kushirikiana na Kenya na Uganda mwaka 2027.