Uongozi wa Simba SC umeweka wazi kuwa furaha inarejea kwa mtindo mwingine ndani ya kikosi hicho, kutokana na mipango makini katika mechi za ushindani kitaifa na kimataifa.

Ikumbukwe kwamba Simba Sc ni miongoni mwa timu zinazoshika nafasi ya tatu za juu katika msimamo wa Ligi Kuu msimu huu, huku ikishikilia rekodi ya kufungwa mabao mengi kwenye mchezo mmoja iliposhuhudia ubao wa Uwanja wa Mkapa ukisoma Simba 1-5 Young Africans.

Jana Alhamis (Januari 25) wachezaji walitarajiwa kuanza mazoezi katika Viwanja vya Mo Arena ikiwa ni maandalizi ya mechi za Ligi Kuu Bara, Ligi ya Mabingwa Afrika kikosi kikiwa chini ya Abdelhak Benchikha ambaye ni kocha mkuu.

Ahmed Ally, Meneja wa ldara ya Habari na Mawasiliano Simba SC amesema kuwa mipango ipo vizuri na furaha inarejea kwa mtindo mwingine.

“Tutarejea kwenye ule ubora wetu na furaha itakuwa kwa Wanasimba kutokana na maandalizi ambayo tunayafanya pamoja na wachezaji kuwa na kiu ya kupata matokeo.

“Wachezaji wakubwa wapo kwenye timu kubwa, hii inamaanisha kwamba wapo tayari kufanya makubwa kwenye mechi zetu zote” amesema Ahmed Ally.

Klopp kung'atuka Liverpool
AFCON 2027 – TFF yaitwa mezani kuyajenga