Kivumbi cha Ligi Kuu Tanzania Bara kinatarajiwa kuendelea tena baada ya kusimama kwa takribani mwezi mmoja kupisha michuano ya Kombe la Mapinduzi 2024 na Kombe la Mataifa ya Afrika ‘AFCON 2023’.

Akizungumza jijini Dar es salaam, Ofisa Habari wa Bodi ya Ligi ‘TPLB’ Karim Boimanda amesema wanatarajia kutoa ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara muda wowote kuanzia leo Jumatatu (Januari 29).

“Ratiba nategemea itatoka muda wowote kuanzia leo Jumatatu (JAnuari 29), maana Taifa Stars imeshatolewa na wachezaji waliobaki AFCON 2023 wanaocheza Ligi Kuu ni watatu,” amesema Boimanda.

Taifa Stars imetolewa kwenye mashindano ya AFCON 2023 yanayoendelea Ivory Coast na inatarajiwa kuwasili nchini leo Jumatatu (Januari 29).

Wachezaji watatu ambao wapo kwenye majukumu ya timu zao za Taifa ni Aziz Ki (Burkina Faso) na Djigúi Diarra (Mali) ambao timu zao zitacheza kesho Jumanne (Januari 30)  na beki wa Simba SC Henock Inonga (DRC) ambao jana Jumapili (Januari 28) waliibamiza Misri katika mechi ya 16.

Ligi hiyo ilisimama Desemba 23 mwaka jana (2023) na mchezo wa mwisho kuchezwa ulikuwa ni kati ya Tabora United na Young Africans uliochezwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma ambapo Young Africans ilishinda bao 1-0 na kukamilisha raundi ya 14.

Mashabiki wana kiu ya kuona ligi ikirejea pamoja na kuona wachezaji waliosajiliwa dirisha dogo.

Gamondi anautaka ubingwa ASFC
MAKALA: Paka bado hawaamini macho yao