Uongozi wa Azam FC, umeweka wazi kuwa unaamini kurejea kwa mastaa wao ambao walikuwa na kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania utazidi kuboresha maandalizi ya kikosi hicho katika vita yao ya kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu 2023/24.

Kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara Azam FC wanakamatia nafasi ya kwanza wakiwa wamekusanya pointi 31 katika michezo 13, huku wakifuatiwa kwa ukaribu na Mabingwa watetezi Young Africans ambao wamekusanya pointi 30 kwenye michezo yao 11, huku Simba wao wakiwa wamekusanya wamefanya na 23 baada ya kucheza michezo 10.

Kwa sasa Benchi la ufundi chini ya kocha Yusuf Dabo wameanza kuandaa programu mbalimbali kwa ajili ya mastaa wote ili kujiwinda na ligi ambayo itarejea rasmi mwanzoni mwa mwezi ujao.

Baada ya kuondoshwa kwenye mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Ivory Coast, mastaa mbalimbali wa timu ya taifa ya Tanzania wakiwemo watatu wa Azam FC ambao ni Sospeter Bajana, Feisal Salum na Lusajo Mwaikenda.

Ofisa Habari wa Azam FC, Hashim Ibwe amesema kama Watanzania wamesikitishwa na kutolewa kwa timu ya Taifa katika mashindano ya ‘AFCON 2023’.

“Kama wadau wa soka nchini tumesikitishwa na matokeo ya Taifa Stars katika mashindano ya AFCON, lakini tunaamini kuwa tutajipanga kwa ajili ya wakati mwingine.

“Kwa sasa kama timu tunaangalia ratiba iliyo mbele yetu na tayari kocha mkuu anaandaa programu ya pamoja ikiwajumuisha wachezaji wetu waliokuwa kwenye majukumu ya timu ya Taifa ili kuendeleza vita ya kusaka ubingwa msimu’ huu.” amesema Ibwe

Pacome aongezewa dozi Young Africans
Mradi mpango wa Mattei kuinufaisha Tanzania