Ademola Lookman amesema juhudi za pamoja za wachezaji wenzake wa Nigeria ndizo zilizofanikisha ushindi wa ‘Super Eagles’ wa mabao 2-0 dhidi ya Cameroon ambao uliwasaidia kutinga Robo Fainali ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika ‘AFCON 2023’.

Lookman alifunga mabao mawili Nigeria ilipoilaza Cameroon kwenye Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny mjini Abidjan na kutinga Robo Fainali juzi Jumamosi (Januari 27).

Lookman, ambaye alitajwa kuwa mchezaji bora wa mechi hiyo, alisema: “Wow, tuna furaha sana kufuzu robo fainali. Tunapocheza pamoja zaidi, ndivyo tunavyozidi kuwa wazuri. Nimesimama hapa sasa, lakini tuzo hii inaakisi utendaji wa timu nzima.”

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26, anafurahia uzoefu wake wa kwanza wa michuano ya AFCON kwa kusema: “Ninapenda hali hii, ni ya ajabu. Mashabiki wetu walitusukuma hadi mwisho kwa sababu hii tukaishinda Cameroon, na unapovaa jezi ya Super Eagles, baadhi ya michezo inasikika zaidi.”

ljumaa wiki hii, Nigeria itacheza na Angola katika mechi ya Robo Fainali, baada ya Swala Weusi hao kuwafunga Namibia mabao 3-0 katika mchezo wa mapema Jumamosi.

Lookman aliongeza: “Angola ni timu nzuri. Tutaichambua na kujiandaa. Kadri unavyozidi kwenda ndivyo inavyokuwa ngumu ndivyo tutakavyochukulia mchezo baada ya mchezo.”

Nigeria inatafuta taji lake la nne na la kwanza katika michuano hiyo tangu mwaka 2013.

JKT imeonesha ishara ya kujali - Dkt. Tax
KMC watambia usajili wa Chilunda