Mlinda Lango wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Lionel Mpasi, anatumai nchi yake itarudia mafanikio yao katika Fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) 2009 kwa kutwaa ubingwa kwenye Fainali za Mataifa Afrika ‘AFCON 2023’, nchini Ivory Coast.

Mpasi alifunga Penati ya ushindi na kuisaidia Congo kuiondoa Misri kwenye ‘AFCON 2023’ hatua ya 16 bora Jumapili (Septemba 28).

Mlinda Lango huyo tayari analinganisha mbio zao katika Fainali za ‘AFCON 2023’ sawa na mafanikio yao ya CHAN nchini Ivory Coast miaka 15 iliyopita.

“Tayari tutapumzika vizuri na kisha tutaichukua mechi baada ya mechi. Haya yote bila kusahau kwamba DR Congo ilishinda taji la mataifa ya Afrika nchini Ivory Coast (CHAN mwaka 2009). Labda hiyo ni ishara,” amesema

Mlinda Lango huyo alieleza jinsi alivyomzuia Gabaski kufunga Penati yake na mbinu nyuma ya Penati yake ya ushindi.

“Nilijaribu kuwa mtulivu. Nilijaribu kumvuruga Gabaski kwenye shuti lake na nikafaulu. Baada ya hapo, nilijikita katika kuweka mbinu yangu sawa,” amesema kipa huyo wa DR Congo.

Mpasi amesema amekumbuka shuti alilokosa akiwa mazoezini na kujaribu kufanya vizuri zaidi.

“Kabla ya kupiga shuti lile, nilifikiria jinsi nilivyokosa nikiwa mazoezi, lakini usiku ule nilifanikiwa,” amebainisha.

Chasambi apewa mbinu za kuishi Simba SC
Taifa Stars yapongezwa AFCON 2023