Kiungo Mshambuliaji wa zamani wa Simba SC, Shiza Ramadhan ‘Kichuya’ amemng’ata sikio winga mpya wa timu hiyo, Ladack Chasambi kuwa kama anataka kufika mbali basi anapaswa kuwasikiliza nyota wazoefu aliowakuta watamfundisha vingi.

Amesema kuwa kinda huyo ameingia Simba SC ameikuta timu ikiwa imekamilika hivyo anatakiwa kupambana kwani tofauti na yeye wakati anatua mitaa ya Msimbazi walikuwa wanajitafuta.

“Simba SC iko tayari sio kama ile waliyokuwa wanaunga unga, Ladack ni mchezaji mzuri atulize akili ajue nini anatakiwa kufanya na wanasimba wanahitaji nini kutoka kwake atafika anapotakiwa kufika.

Lakini asiweke presha kubwa maana bado ni kijana mdogo ameenda kwenye timu kubwa umri wake na alipoenda ni vitu viwili tofauti, anatakiwa kupambana zaidi ya alipotoka,” amesema Kichuya

Amesema asijipe ukubwa anatakiwa ajue yeye bado ni mdogo anatakiwa kujifunza afanye kazi kwani miongoni mwa vijana ambao Mkoa wa Morogoro wanajivunia nao ni yeye na wanaamini kwa kipaji alichonacho ataisaidia Simba SC.

Mjerumani anaitaka Black Stars
Lionel Mpasi: DR Congo itarudia ya 2009