Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Misri, Rui Vitoria ameshindwa kueleza hatima yake baada ye timu yake kutolewa katika hatua ya 16 bora ya Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika ‘AFCON 2023’, akilaumu kukosa bahati kwao.

Misri ambao ni mabingwa mara saba wa AFCON 2023 wametolewa juzi Jumapili (Januari 28) baada ya timu yao kufungwa na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kwa Penati 8-7.

Timu hizo zilitoka sare ya kufungana bao 1-1 katika muda wa kawaida huku Misri wakimaliza mchezo wakiwa na wachezaji 10 baada ya kutolewa kwa Mohamed Hamdy katika kipindi cha pili cha muda wa yongeza. Misri inaondoka Ivory Coast bila ya kushinda mchezo hata mmoja.

Hiyo ni sare ya nne mululizo kwao katika AFCON 2023, na niya sita ukihesabu na zile za mashindano yaliyopita yaliyofanyika nchini Cameroon, pia ni mechi ya tano mfululizo kwenda hadi muda wa nyongeza katika hatua ya mtoano.

Alipoulizwa kuhusu mustakabali wake na Misri katika mkutano na waandishi wa habari baada ya mechi, Vitoria alisema: “Huu si wakati wa kufanya maamuzi ya haraka, tutafikiri kabla ya uamuzi wowote,” alisema Vitoria alipoulizwa kuhusu hatima yake.

“Wachezaji walikuwa wazuri, na hii ndio soka, kuna wakati wa furaha na huzuni.

“Tuliiandaa timu yetu kwa ajili ya ‘AFCON 2023’, lakini wakati unapofanya juhudi zote na matokeo sio yale uliyotarajia. Tunahitaji kuangalia hatima yetu kuhusu mipango ya baadae.”

Baada ya kukosa taji la Afrika tangu mwaka 2010, Vitoria alishindwa kusema hatima yake.

“Hatuwezi kuwa kama hivyo, historia imedhihirisha kuwa Misri ni timu kubwa, lakini inapitia mabadiliko makubwa. Tunatakiwa kujenga msingi imara na bila shaka tutakuwa imara mbeleni,” amesema.

Wakati huo huo, beki wa zamani wa timu ya taifa ya Misri, Wael Gomaa amemtupia lawama Vitoria kwa timu hiyo kushindwa kufanya vizuri katika mashindano hayo mwaka huu.

UVCCM wamuunga mkono Dkt. Samia fomu ya Urais
Benchikha: Mapambano lazima yaendelee